Uyui FM Radio

Kamati ya siasa Uyui yaridhishwa na mradi wa maji

26 September 2024, 10:40 am

Viongozi wa kamati ya siasa wakimtwisha ndoo ya maji mmoja wa wananchi.Picha na Mohamed Habibu

Kamati ya siasa ya Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Uyui inafanya ziara ya ufuatiliaji na ukaguzi wa miradi inayotekelezwa na serikali katika majimbo ya Tabora Kaskazini na Igalula.

Na Nyamizi Mdaki

Kamati ya siasa ya Halmashauri kuu ya CCM Wilayani Uyui Mkoani Tabora imeridhishwa na utekelezaji wa mradi wa maji katika kata ya Nsimbo.

Akizungumza akiwa kwenye mradi huo Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Uyui Rubasha Makoba amesisitiza utunzwaji wa mradi huo.

Mwenyekiti Rubasha akizungumza.Picha na Mohamed Habibu
Sauti ya Makoba

Naye Mbunge wa Tabora Kaskazini Almas Maige amesema Mradi huo ni sehemu ya mradi wa maji kutoka ziwa Victoria.

Mbunge Maige akizungumza na wananchi pamoja na viongozi.Picha na Mohamed Habibu
Sauti ya mbunge Maige

Akimwakilisha Meneja wa RUWASA Wilaya ya Uyui kusoma taarifa ya mradi huo wa maji kutoka mayombo kwenda Nsimbo Charles Isaya amesema