ACP Deleli: Waathirika zaidi wa ajali ni bodaboda
12 July 2024, 5:45 pm
Chuo cha mafunzo ya udereva Utalii East Afrika – Tabora kimeratibu mafunzo bure kwa waendesha Bodaboda,bajaji na maguta zaidi ya 500 Manispaa ya Tabora kwa kipindi cha mwezi 1 kwa lengo la uzingatiaji wa sheria za usalama barabarani.
Na Zaituni Juma
Waendesha pikipipiki za abiria maarufu kama Bodaboda wametajwa kuwa, ndio waathirika zaidi wa ajali za barabarani nchini ukilinganisha na watumiaji wengine wa barabara.
Mkuu wa dawati la elimu ya usalama na mafunzo barabarani Tanzania ACP Michael Deleli amesema hayo wakati akizungumza kwenye hafla ya kufunga mafunzo ya watumiaji wa vyombo vya moto yaliyofanyika eneo la machinga Complex Manispaa ya Tabora.
Kwa upande wake mkurugenzi wa chuo cha Utalii cha East Afrika Tabora Shabani Mrutu amesema mafunzo hayo yatasaidia kupunguza ajali za barabarani ambazo zinaleta athari kubwa kwa vijana na jamii kwa ujumla.
Baadhi ya wahitimu wa mafunzo hayo Elizaberth Bimla na Isaya Ibrahimu wamesema wamepata uelewa wa kutosha juu ya matumizi sahihi ya alama za barabarani tofauti na hapo awali.