Uyui FM Radio

COASCO yatakiwa kudhibiti mali za ushirika

2 July 2024, 4:25 pm

Baadhi ya wananchi na viongozi waliohudhuria wiki ya ushirika.Picha na Mohamed Habibu

Maadhimisho ya wiki ya ushirika duniani kitaifa yamefanyika mara nne mfululizo katika viwanja vya Nanenane Ipuli Manispaa ya Tabora.

Na Zaituni Juma

Naibu Waziri wa Kilimo David Silinde amelitaka Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika- COASCO kuendelea kuimarisha mifumo ya udhibiti na usimamizi wa mali zikiwemo fedha za vyama vya ushirika.

Naibu Waziri Silinde ametoa agizo hilo wakati akimwwakilisha Waziri wa Kilimo kwenye uzinduzi wa maadhimisho ya Wiki ya Ushirika Duniani yanayofanyika kitaifa mkoani Tabora.

Naibu Waziri wa Kilimo Silinde akizungumza na wananchi. Picha na Mohamed Habibu
Sauti ya Naibu Waziri

Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Dkt. Benson Ndiege amesema wanafanya ukaguzi na kuchukua hatua kwa viongozi wanaokiuka sheria na taratibu zilizowekwa.

Akimwakilisha Mkuu wa Mkoa, Mkuu wa Wilaya ya Tabora Deusdedith Katwale amesema maadhimisho ya ushirika kufanyika kitaifa mkoani hapa kumeongeza chachu ya maendeleo kwa wananchi.

Mkuu wa Wilaya Katwale akizungumza na wananchi. Picha na Mohamed Habibu
Sauti ya Mkuu wa Wilaya Katwale