Milioni 561 za punguza msongamano madarasani
6 May 2024, 1:03 pm
Katika mwaka wa fedha 2022/2023 Manispaa ya Tabora ilipokea bilioni 1.8 kupitia mradi wa boost kwaajili ya kujenga shule mpya 3 na zingine kukarabatiwa.
Na Mohamed HabibuJumla ya shilingi milioni 561 zimetumika kujenga shule ya msingi KIDATU Manispaa ya Tabora ili kupunguza msongamano wa wanafunzi katika shule ya msingi Magereza.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Tabora ELIAS KAYANDABILA amesema, hayo wakati wa ziara yake shuleni hapo kwa lengo la kufuatilia ufundishaji na maendeleo ya wanafunzi kwa ujumla.
Kwaupande wake mwalimu mkuu wa shule ya msingi Kidatu IMANI SANKE amesema shule hiyo ina vyumba vya madarasa 14,matndu ya vyoo 18 pamoja na jengo la elimu ya awali lenye vyumba viwili vya madarasa.
Nao baadhi ya wazazi NEEMA CHAKOKO na HAMZA JUMA wameipongeza serikali kwa kukamilisha mradi huo kutokana na changamoto za awali ikiwemo ikiwemo wanafunzi kutembea umbali mrefu na msongamano mkubwa madarasani.