Klabu za usalama barabarani zapunguza ajali kwa wanafunzi Tabora
17 January 2025, 4:41 pm
katibu wa kamati ya ushauri ya watumiaji huduma za usafiri ardhini mkoa wa Tabora LATRA CCC Joakim Milambo amesema ni kuhakikisha wanapanua wigo wa elimu ya usalama barabarani
Na Nyamizi Mdaki
Uanzishwaji wa Klabu za usalama barabarani kwa wanafunzi katika baadhi ya shule mkoani Tabora kumesaidia kupunguza ajali za barabarani kwa wanafunzi wanapokwenda na kutoka shuleni.
Hayo yameelezwa na Mlezi wa mafunzo ya klabu hiyo kutoka shule ya Msingi Ipuli inayosimamiwa na Kamati ya ushauri ya watumiaji huduma za usafiri ardhini LATRA CCC Mwalimu Fatma Kitentye.
Akieleza malengo ya klabu hiyo katibu wa kamati ya ushauri ya watumiaji huduma za usafiri ardhini mkoa wa Tabora LATRA CCC Joakim Milambo amesema ni kuhakikisha wanapanua wigo wa elimu ya usalama barabarani.
Katika hatua nyingine Joakim amewataka waendesha vyombo vya usafiri kuacha kupandisha nauli kwa kigezo cha kuongezeka uhitaji wa usafiri huo baada ya shule kufunguliwa.