Uyui FM Radio

DC Magembe atangaza vita dhidi ya ‘chagulaga’

16 January 2025, 1:09 pm

Baadhi ya wanawake waliohudhuria hafla ya utoaji wa mikopo ya halmashauri.Picha na Zaituni Juma

Wananchi wamesisitizwa kutoa ushirikiano kwa vyombo vya usalama ili kutokomeza utamaduni huo.

Na Zaituni Juma

Mkuu wa Wilaya ya Sikonge Cornel Magembe amekemea vikali utamaduni wa baadhi ya wanaume kuwalazimisha wasichana wadogo kuingia nao kwenye mahusiano ya kimapenzi maarufu kama chagulaga jambo ambalo ni kinyume na sheria.

Akizungumza katika hafla ya utoaji mikopo kwa vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu awamu ya kwanza kwa mwaka 2024-2025, ameagiza vyombo vya usalama kufanya operesheni kwenye maeneo ya minada na sherehe mbalimbali ili kudhibiti suala hilo.

Mkuu wa Wilaya akiongea na viongozi pamoja na wananchi wa wilaya ya Sikonge. Picha na Zaituni Juma
Sauti ya DC Magembe

Mkuu wa Wilaya Magembe amesema hadi sasa wameshakamatwa baadhi ya vijana wenye tabia hiyo na wamehukumiwa kifungo cha miezi 6 jela.

Sauti ya DC Magembe