Uyui FM Radio

Mbolea ya CAN yaota mbawa Tabora

8 January 2025, 10:33 am

Mwenyekiti wa jukwaa la Ushirika Mkoa wa Tabora Hamisi Katabanya akizungumzia ukosefu wa mbolea ya CAN

Wakulima wa zao la Tumbaku wanaendelea na sintofahamu wakati wakielekea kwenye kuvuna zao hilo

Na Nyamizi Mdaki

Mwenyekiti wa jukwaa la Ushirika Mkoa wa Tabora Hamisi Katabanya amesema kwamba wakulima wa Tumbaku wanahofia kupata hasara mwaka 2024/2025 wa kilimo kufuatia kukosa pembejeo ya mbolea ya KANI.

Amebainisha hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari akisema kwamba wanaeleka kwenye kuvuna lakini bado hawajapata mbolea ya kuboresha mimea hiyo.

Sauti ya Mwenyekiti wa Jukwaa la ushirika Tabora Hamisi Katabanya

Vile vile Mwenyekiti wa chama cha msingi Ikonongo Wilayani Kaliua John Alex anazungumzia changamoto hiyo.

Sauti ya Mwenyekiti wa chama cha msingi Ikonongo Wilayani Kaliua John Alex

Aidha wakulima hao wamemuomba Mkuu wa Mkoa wa Tabora Paul Chacha asaidie upatikanaji wa mbolea hiyo ya kani.