Uyui FM Radio

Wanafunzi  27,114 kurudishwa shuleni kuendelea na masomo

5 November 2024, 4:07 pm

Baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Kidatu wakiwa darasani.Picha na Mohamed Habibu

Wanafunzi hao wanaotakiwa kurudi shuleni kuendelea na masomo ni wa shule za msingi pekee zilizopo mkoani Tabora

Na Zaituni Juma

Serikali  mkoani  Tabora imedhamiria kuwarudisha shuleni Jumla ya wanafunzi  elfu 27,114 wa shule za msingi ambao wako  nje ya mfumo wa taalama  kwa sasa.

Akizungumza na waandishi wa habari kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Tabora Paul Chacha, Mkuu wa Wilaya ya Urambo Dkt. Khamis  Mkanachi amesema, watashirikiana na viongozi kuanzia ngazi za vitongoji kuhakikisha watoto hao wanarudi shuleni.

DC Mkanachi akizungumza na waandishi.Picha na Nicholaus Mwaibale
Sauti ya Mkanachi

Nae Kaimu afisa elimu mkoa wa Tabora  mwalimu Alon Vedasco amesema wameanzisha kampeni hiyo maalumu ili kuhamasisha jamii kuona umuhimu wa kuwapelea shule watoto wao.

Kaimu afisa elimu mkoa wa Tabora  mwalimu Alon akizungumza.Picha na Zaituni Juma
Sauti ya mwalimu Alon

Kwa mujibu wa mkuu wa wilaya Mkanachi ambae amemuwakilisha mkuu wa mkoa Paul Chacha amesema kuanzia disemba 2 mwaka huu itafanyika kampeni ya nyumba kwa nyumba kuwabaini wanafunzi waliocha shule ili kuwarudisha kuendelea na masomo.