Uyui FM Radio

Tabora United kupewa milioni 10 kwa kila mechi

21 May 2024, 10:05 pm

Tabora United imesalia na Michezo Mitatu Mmoja ikicheza nyumbani dhidi ya Ihefu Sc na michezo miwili ugenini dhidi ya Yanga na Namungo.

Na Mohamed Habib

Mkuu wa mkoa wa Tabora Paul Chacha ameahidi kutoa shilingi Milioni 10 ikiwa ni Hamasa kwa klabu ya Tabora United katika Michezo mitatu iliyosalia katika Ligi kuu ya NBC ambapo kila mechi watayoshinda watakabidhiwa shilingi milioni 10.

Chacha Amesema nidhamu ya kujitoa kwa Wachezaji ndani ya kiwanja itasaidia timu kupata matokeo na kusalia katika Ligi ya NBC, hivyo ameongeza kuwa Tabora United ikipata ushindi katika mchezo wao na Ihefu basi atongeza dau ambalo hajaliweka wazi kuwa ni kiasi gani nje ya Million 10 aliyothibitisha kuitoa baada ya ushindi.

Mkuu wa mkoa Paul Chacha akizungumza na Wachezaji wa Tabora United. Picha na Mohamed Habibu

Sautu ya mkuu wa mkoa wa Tabora Mhe. Paul Chacha

Tabora United inahitaji kushinda mchezo wa kesho ili kufufua matumaini ya kusalia ligi ya NBC, Tabora United imesalia na Michezo Mitatu Mmoja ikicheza Nyumbani dhidi ya Ihefu Sc na Michezo miwili ugenini Dhidi ya Yanga na Namungo.