RC Tabora akemea rushwa kwenye michezo
8 January 2025, 11:38 am
Mkuu wa Mkoa wa Tabora asema rushwa inashusha hadhi ya wachezaji pamoja na timu.
Na Zabron George
Wachezaji wa timu ya Tabora united wameshauliwa kutopokea chochote kutoka kwa mtu mwenye lengo la kuuza mchezo kwani kufanya hivyo kutashusha hadhi ya wachezaji pamoja na timu nzima kwa ujumla
Ushauri huo umetolewa na mkuu wa mkoa wa Tabora paul chacha alipo watembelea kwenye uwanja wa mazoezi ambapo pia amewaahidi kuendelea kuwashika mkono kuwatia moyo katika michezo mbalimbali
Kwa upande wake nahodha wa timu hiyo Kelvin Kingu akizungumza kwa niaba ya wenzake amemshukuru paul chacha kwa mchango anaoutoa kuhakikisha timu inapata matokeo mazuri ndani ya uwanja
Timu ya Tabora united imekuwa na mwendelezo mzuri kwenye ligi kuu tanzania bara baada ya kuzifunga timu vigogo ikiwemo yanga aliefungwa goli 3 kwa 1 huku azam akifungwa goli 2 kwa 1