Uyui FM Radio
Mbolea ya CAN yaota mbawa Tabora
8 January 2025, 10:33 am
Wakulima wa zao la Tumbaku wanaendelea na sintofahamu wakati wakielekea kwenye kuvuna zao hilo
Na Nyamizi Mdaki
Mwenyekiti wa jukwaa la Ushirika Mkoa wa Tabora Hamisi Katabanya amesema kwamba wakulima wa Tumbaku wanahofia kupata hasara mwaka 2024/2025 wa kilimo kufuatia kukosa pembejeo ya mbolea ya KANI.
Amebainisha hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari akisema kwamba wanaeleka kwenye kuvuna lakini bado hawajapata mbolea ya kuboresha mimea hiyo.
Vile vile Mwenyekiti wa chama cha msingi Ikonongo Wilayani Kaliua John Alex anazungumzia changamoto hiyo.
Aidha wakulima hao wamemuomba Mkuu wa Mkoa wa Tabora Paul Chacha asaidie upatikanaji wa mbolea hiyo ya kani.