Wanafunzi 27,114 kurudishwa shuleni kuendelea na masomo
5 November 2024, 4:07 pm
Wanafunzi hao wanaotakiwa kurudi shuleni kuendelea na masomo ni wa shule za msingi pekee zilizopo mkoani Tabora
Na Zaituni Juma
Serikali mkoani Tabora imedhamiria kuwarudisha shuleni Jumla ya wanafunzi elfu 27,114 wa shule za msingi ambao wako nje ya mfumo wa taalama kwa sasa.
Akizungumza na waandishi wa habari kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Tabora Paul Chacha, Mkuu wa Wilaya ya Urambo Dkt. Khamis Mkanachi amesema, watashirikiana na viongozi kuanzia ngazi za vitongoji kuhakikisha watoto hao wanarudi shuleni.
Nae Kaimu afisa elimu mkoa wa Tabora mwalimu Alon Vedasco amesema wameanzisha kampeni hiyo maalumu ili kuhamasisha jamii kuona umuhimu wa kuwapelea shule watoto wao.
Kwa mujibu wa mkuu wa wilaya Mkanachi ambae amemuwakilisha mkuu wa mkoa Paul Chacha amesema kuanzia disemba 2 mwaka huu itafanyika kampeni ya nyumba kwa nyumba kuwabaini wanafunzi waliocha shule ili kuwarudisha kuendelea na masomo.