Mwalimu atuhumiwa kumlawiti mwanafunzi
1 August 2024, 10:54 am
Jamii imesisitizwa kutoa taarifa za vitendo vya ukatili kwa jeshi la polisi ili vishughulikiwe.
Na Adela Moses
Mtoto mwenye umri wa miaka saba mwanafunzi wa shule ya Mtakatifu Doroth Manispaa ya Tabora amedaiwa kulawitiwa na mwalimu wake.
Hayo yamebainishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora Kamishna Msaidizi Mwandamizi Richard Abwao wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya tukio hilo.
Sheria za nchi ya Tanzania zinaonya vikali vitendo vya ulawiti kama ambavyo anafafanua mwanasheria.
Nao viongozi wa dini wametoa maelekezo na msisitizo kwa jamii juu ya kuepuka vitendo vya ukatili ikiwemo ulawiti.
Afisa Ustawi wa Jamii kutoka hospitali ya rufaa ya mkoa wa Tabora Kitete Johari Mohamedi amesema madhara yanayoweza kutokea endapo mtu atalawitiwa ni pamoja na kuathirika kisaikolojia.