Uyui FM Radio

Uboreshaji miundombinu wakuza sekta ya elimu Tabora

30 July 2024, 6:19 pm

Muonekano wa madarasa katika shule mpya ya msingi Kidatu Manispaa ya Tabora.Picha na Mohamed Habibu

Bilioni 31 zimetolewa na serikali kuu kwa ajili ya ujenzi wa shule mpya za msingi, Sekondari, vyumba vya madarasa na nyumba za Walimu mkoani Tabora.

Na Nicholaus Mwaibale

Mkoa wa Tabora umepiga hatua kubwa katika sekta ya Elimu katika kipindi cha miaka mitatu mfululizo kutokana na uboreshaji wa miundo mbinu ya shule, jitihada za Walimu na usimamizi mzuri.

Akizungumza na UFR ofisini kwake, Katibu Tawala msaidizi mkoa wa Tabora anayeshughulikia sekta ya elimu Mwalimu Juma Kaponda amesema ufaulu umeongezeka kwa kiwango kikubwa ikilinganishwa na miaka ya nyuma.

Mwalimu Juma Kaponda akizungumza.Picha na Mohamed Habibu
Sauti ya Mwalimu Kaponda

Mwalimu Kaponda amesema katika kipindi hicho ufaulu Bora umeongezeka kutoka asilimia 0.2 mwaka 2021 hadi kufikia asilimia 1.5 mwaka 2023.

Baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Kidatu wakiwa darasani.Picha na Mohamed Habibu
Sauti ya mwalimu Juma Kaponda