Dkt. Msonde: Walimu wekeni msingi mzuri wa lugha ya kiingereza
30 June 2024, 9:10 pm
Dkt. Charles Msonde amekuwa na ziara katika mikoa mbalimbali ikiwemo Kagera na Tabora ambapo pamoja na mambo mengine ametumia fursa hiyo kuzungumza na walimu.
Na Elisha Lusatila
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais – TAMISEMI (Elimu) Dkt. Charles Msonde amewataka walimu mkoani Tabora kuweka msingi mzuri kwa wanafunzi katika ufundishaji wa lugha ya kingereza ili wasipate changamoto wakifka elimu ya sekondari.
Dkt. Msonde amesema hayo wakati akizungumza na walimu, walimu wakuu, wakuu wa shule, maafisa elimu wa kata na wilaya pamoja na wasimamizi wa elimu katika wilaya ya Uyui kwenye ukumbi wa shule ya sekondari Idete iliyopo wilayani humo.
Awali Mkuu wa Wilaya ya Uyui Zakaria Mwansasu ameiomba serikali kuongeza nguvu kwenye vituo shikizi vilivyopo wilayani Uyui ili kuepuka utoro kwa wanafunzi kutokana na kutembea umbali mrefu.