RC Chacha akabidhi milioni 50 Tabora United
21 June 2024, 7:39 pm
Kiasi cha shilingi milioni 50 kilichotolewa kwa wachezaji na viongozi wa timu ya Tabora United ni utekelezaji wa ahadi aliyotoa RC Chacha kwa timu hiyo kama itafanya vizuri katika michezo ya mtoano na kubakia ligi kuu.
Na Mohamed Habibu
Mkuu wa mkoa wa Tabora Paul Chacha amekabidhi shilingi million 50 kwa klabu ya Tabora United ikiwa ni pongezi baada ya kusalia ligi kuu ya NBC.
Chacha amekabidhi kiasi hicho katika hafla ya kupongeza Benchi la ufundi Wachezaji na Viongozi waliopambana katika kuhakikisha timu inasalia katika mashindano ya Ligi Kuu NBC.
Akizungumza katika hafla hiyo RC Chacha amewapongeza Viongozi, Kocha na Wachezaji kwa kushikamana na kupambana ipasavyo katika michezo yao na hatimaye kufanya vizuri.
Mkuu wa mkoa Chacha akizungumza na Wachezaji pamoja uongozi wa Tabora United. Picha na Mohamed Habibu
Sauti ya mkuu wa mkoa wa Tabora Mhe. Paul Chacha
Naye Kamanda wa polisi Mkoa wa Tabora SACP. Richard Abwao ambaye ni Mwenyekiti wa timu hiyo amesema wamejipanga kuboresha uwanja wa Nyumbani ili kuepuka usumbufu wa michezo kuhamishiwa katika mikoa jirani.
Amesisitiza kuwa wanajipanga kufanya usajili wa Wachezaji wapya ili kuimarisha kikosi hicho katika mashindano Ya Ligi kuu NBC.
Kamanda wa polisi mkoa wa Tabora SACP Abwao akizungumza na Wachezaji pamoja uongozi wa Tabora United. Picha na Mohamed Habibu
Sauti ya Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora
Pia kamanda Abwao Amesema klabu inaheshimu mikataba ya Wachezaji na taratibu za kuvunja ama kuendelea zitafutwa ili kuiepusha timu kupewa adhabu na shirikisho la kabumbu ulimwenguni Fifa.