Uyui FM Radio

TANESCO kufanya maboresho ya mfumo wa LUKU

30 May 2024, 2:50 pm

Muonekano wa Mita za LUKU.picha na Mohamed Habibu

Mita za LUKU ni mfumo wa kulipia umeme kadiri mteja anavyotumia huku zaidi ya wateja laki 1 wakitarajiwa kufanyiwa maboresho  kwenye mfumo wa huo.

Na Zaituni Juma

Shirika la Umeme Tanzania TANESCO  Mkoa wa Tabora linatarajia kufanya maboresho ya mfumo wa LUKU kuanzia  juni  mosi  mwaka huu ili kuongeza ufanisi na usalama katika mfumo huo

Afisa Tehama mwandamizi wa shirika hilo Mkoa wa Tabora Peter Mbaga amebainisha hayo wakati akizungumza na kituo hiki juu ya maboresho ya mfumo wa LUKU yatakavyofanyika.

Afisa Tehama mwandamizi Peter Mbaga akiwa studio za UFR .Picha na Mohamed Habibu
Sauti ya Afisa TEHAMA Mwandamizi Mbaga

Nae afisa Mahusioano TANESCO mkoa wa Tabora MWANAHAMISI  HUSSEIN  amesema, maboresho hayo hayana  athari yoyote  katika matumizi ya mteja.

Afisa Mahusiano TANESCO – Tabora Mwanahamis akizungumza kupitia UFR.Picha na Mohamed Habibu