Bomoabomoa yawafikia waliovamia hifadhi ya barabara Tabora
28 May 2024, 5:39 pm
Kwa mujibu wa sheria ya ardhi kifungu namba 6 na sheria ya barabara namba 13 ya mwaka 2007 na kanuni ya mwaka 2009 kifungu cha 29 kwa pamoja vinaeleza umuhimu wa kutunza na kuheshimu hifadhi hizo.
Na Zaituni Juma
Wakala ya Barabara Nchini TANROADS mkoa wa Tabora imetoa siku 30 kwa wananchi waliovamia kujenga nyumba na vibanda kwenye barabara ya Ushokola kaliua mjini hadi Kasungu kuhakikisha wanabomoa kwa hiari yao wenyewe.
Akizungumza na wananchi wanaoishi kwenye maeneo hayo,Msimamizi wa TANROADS mkoa wa Tabora Mhandisi Enock Mitenda amesema baada ya muda huo kumalizika hatua zitachukuliwa kwa watakao kiuka.
Kwa upande wake diwani wa kata ya Kaliua NESTORY ELIAS amekiri kuwa uvamizi huo wa hifadhi ya barabara ni kosa hivyo watasimamia utekelezaji wa suala hilo pasipo kuathiri mwananchi yoyote.