Zaidi ya wasichana 200,000 kufikiwa na chanjo ya HPV Tabora
23 April 2024, 7:10 pm
Kampeni ya kuzuia saratani ya mlango wa kizazi kwa wasichana wenye umri wa miaka 9 hadi 14 imezinduliwa nchini naitafanyika kwa siku 5 mfululizo.
Na Mohamed Habibu
Wazazi na walezi wenye wasichana walio na umri wa miaka 9 hadi 14 mkoani Tabora wametakiwa kuwaruhusu kupata chanjo ya kuzuia saratani ya mlango wa kizazi ili kuwaepusha na maambukizi ya ugonjwa huo.
Mkuu wa mkoa wa Tabora Paulo chacha amesema hayo wakati wa uzinduzi wa chanjo hiyo uliofanyika shule ya msingi kizigo iliyopo Manispaa ya Tabora.
Kwa upande wake Afisa elimu Mkoa wa Tabora JUMA KAPONDA amesema kuwa walimu mkoani hapa wako tayari kuwapa ushirikiano wataalam wa afya huku akiwasisitiza wazazi kuiamini serikali.
Hata hivyo mkuu wa mkoa Paul Chacha amezitaka Taasisi binafsi pamoja na umma kushirikiana kuelimisha jamii juu ya umuhimu wa afya.