Asilimia 90 kesi zinazoripotiwa mahakama ya wilaya Uyui ni za ubakaji
31 January 2024, 1:29 pm
Asilimia 90 ya kesi zinazoripotiwa katika mahakama ya Wilaya ya Uyui Mkoani Tabora ni za ubakaji.
Na Zaituni Juma
Hakimu mkazi Mfawidhi Mahakama ya wilaya ya Uyui mkoani Tabora Tausi Mongi amesema asilimia 90 ya kesi zinazoripotiwa katika mahakama hiyo ni za ubakaji.
Akizungumza kwenye kipindi cha Kifungua Kinywa, Mongi amesema kwamba kesi hizo husababishwa na uelewa mdogo wa masuala ya sheria.
Kwa upande wake Hakimu mkazi mfawidhi mahakama ya mwanzo Upuge wilayani Uyui Jackline Lukuba amewasihi wananchi kuhudhuria viwanja vya mahakama ya wilaya pamoja na zile za mwanzo kupata elimu bure ya sheria.
Kauli mbiu ya wiki ya sheria mwaka 2024 ni umuhimu wa zana ya haki kwa ustawi wa Taifa, nafasi ya mahakama na wadau katika kuboresha mfumo jumuishi wa haki jinai.