Mufti ahimiza waislam kushirikiana na serikali
7 October 2021, 7:53 pm
Mufti Mkuu wa Tanzania sheikh Abubakar Zubeir Ally amewataka viongozi wa dini ya kiislam mkoani Tabora kuendeleza ushirikiano na viongozi wa serikali ili kuhakikisha wanafanya kazi kwa ufanisi, weledi pamoja na kuzingatia madili ya dini.
Wito huo ameutoa mjini Tabora wakati akizungumza na viongozi wa dini, serikali pamoja na waumini wa dini ya kiislam kwenye ukumbi wa isike Mwana kiyungi kufuatia ziara yake ya kikazi ya siku tatu mkoani Tabora.
Awali mkuu wa mkoa wa Tabora Dokta Batilda Buriani amemkaribisha Mufti mkuu wa Tanzania mkoani Tabora huku akisema kuwa mkoa bado unafursa nyingi hivyo katika miradi mbalimbali ya kimkakati ikiwemo Reli ya kisasa na Bomba la mafuta ghafi.
Naye Sheikh wa mkoa wa Tabora Ibrahim Mavumbi amesema kuwa Ujio wa Mufti ni njia moja wapo ya kuendelea kufahamu miradi mbalimbali ya kiuchumi na kijamii iliyopo kwa manufaa mkoa na taifa kwa ujumla.