Rc Tabora awa mbogo kusuasua ujenzi wa hospital ya Wilaya
26 April 2021, 5:45 pm
Mkuu wa mkoa wa Tabora Dkt Philemon Sengati ameiagiza Wilaya ya Kaliua kukamilisha haraka mradi wa hospitali ya wilaya hiyo pamoja na ujenzi wa kituo cha afya Usinge ili wananchi waanze kupata huduma za afya maeneo hayo.
Ametoa agizo hilo akiwa kwenye ziara ya kikazi wilayani humo kukagua miradi ya maendeleo ikiwemo ya afya na kuagiza miradi hiyo inapaswa kukamilika kabla ya juni 30 mwaka huu.
Akizungumzia suala hilo mkuu wa wilaya ya Kaliua Abel Busalama amesema miradi hiyo imechelewa kukamilika kwa wakati kutokana na changamoto ya makisio ya vifaa kuwa chini tofauti na mahitaji.
Kwa mujibu wa viongozi hao kukamlika kwa hospitali ya wilaya pamoja na kituo cha afya cha usinge utakuwa na manufaa kwa wananchi kwa kuwaondolea adha ya kutembea umbali mrefu kwa ajili ya huduma za afya.