Katibu Hospitali ya Rufaa Kitete kufanyiwa uchunguzi wa kinidhamu
20 April 2021, 5:41 pm
Watumishi wa afya katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Tabora -Kitete wamemuomba mkuu wa mkoa wa Tabora kufanya uchunguzi wa kinidhamu dhidi ya Katibu wa Hospitali hiyo BABY NYIMBO kutokana na tuhuma mbalimbali za kiutendaji.
Akizungumza kwa niaba ya watumishi wengine wa Hospitali hiyo afisa muunguzi ADELINA ILOGOLA amesema katibu huyo amekuwa ni kero kutokana na kutozingatia misingi ya utumishi.
Kufuatia malalamijko hayo mkuu wa Mkoa wa Tabora Doktari PHILLEMON SENGATI ametoa maagizo katika ofisi ya katibu tawala wa Mkoa kufanya uchunguzi baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa watumishi wa hospitali hiyo.
Aidha katika hatua nyingine Mkuu wa mkoa amesisitiza utendaji wenye maadili ya taaluma hiyo kwa kufuata misingi ya utumishi bora.
Hayo yamejiri baada ya Mkuu wa Tabora Dokta PHILLEMO SENGATI kufanya ziara katika hospitali hiyo kwa lengo la kubaini changamoto zilizopo.