Uyui FM

Wawili wafariki ajali ya lori la vinywaji Tabora

25 November 2026, 10:26 pm

Lori la kampuni ya Nyanza Bottle lenye namba za usajili T127 AUP baada ya Ajali. Picha na Elison Sabuni

Watu wawili wamefariki dunia na mmoja kujeruhiwa baada ya lori Nyanza Bottle, kuacha njia na kupinduka katika eneo la Mayombo, mkoani Tabora.

Na Elison Sabuni

Watu wawili wamefariki Dunia na mmoja kujeruhiwa katika ajali ya barabarani iliyohusisha lori aina ya Scania, lenye namba za usajili T127 AUP, mali ya kampuni ya Nyanza Bottle, kuacha njia na kupinduka katika eneo la Mayombo mkoani Tabora.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora na Mkuu wa Kitengo cha Polisi Jamii Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Mahemba Kavalambi. Picha na Elison Sabuni

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora na Mkuu wa Kitengo cha Polisi Jamii Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Mahemba Kavalambi, amesema chanzo cha ajali hiyo ni dereva kushindwa kumudu lori wakati akishuka kwenye mteremko mkali.

Sauti ya ACP Mahemba
Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Tabora, Kamishna Msaidizi Mwandamizi Loshipay Laizer. Picha na Elison Sabuni

Kwa upande wake, Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Tabora, Kamishna Msaidizi Mwandamizi Loshipay Laizer, amesema walipokea taarifa kutoka Jeshi la Polisi na kufika eneo la tukio kwa ajili ya zoezi la uokoaji.

Sauti ya Loshipay Laizer

Baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Mayombo wameeleza kusikitishwa na tukio hilo huku wakitoa wito kwa madereva kuzingatia sheria za usalama barabarani.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Mayombo, Dina Masalu. Picha na Elison Sabuni

Mwenyekiti wa Kijiji cha Mayombo, Dina Masalu, amesema alipokea taarifa za ajali hiyo kutoka kwa mmoja wa wananchi wake majira ya saa saba usiku na baada ya kufika eneo la tukio alitoa taarifa kwa vyombo vya ulinzi na usalama.

Sauti ya Mwenyekiti Dina Masalu

Ajali hiyo imetokea majira ya saa saba usiku wa kuamkia leo Novemba 25, 2026, katika Kijiji cha Mayombo, Kata ya Magiri, Wilaya ya Uyui mkoani Tabora.