Uyui FM

Uwezo wa mtu utumike kusaidia mtu mwingine

9 September 2025, 9:16 pm

Na Zabron G Balimponya

Jamii mkoani Tabora imeshauliwa kutambua na  kutumia uwezo uliopo katika kila mtu mmoja mmoja ili uwezo huo usaidie kuleta manufaa kwenye maisha na kujali watu wengine .

Wito huo umetolewa na Felista Michael ambae ni muwezeshaji wa elimu ya stadi za maisha Tabora  kutoka shirika la Camfed wakati akizungumza na UFR ambapo amesisitiza kuwa kila mtu ana uwezo ingawa hautumiki kiusahihi

Felista Michael muwezeshaji wa elimu ya stadi za maisha Tabora akiwa studio za Uyui FM Radio

Sauti ya Felista Michaeli

Baadhi ya wakazi wa Manisipaa ya Tabora Elias Habibu na Mariamu Peter wametoa maoni yao juu ya kutambua uwezo hasa kwenye maisha ya kila siku na kutoa ushauli kwa baadhi ya wale ambao hawajatambua uwezo wao

Sauti za Elias Habibu na Mariam Peter

Kwa mjibu wa muwezeshaji wa shirika la Camferd Felista Michael zipo aina 37 za uwezo ambazo binadamu anazo licha ya kuwa ni mara chache mwanadamu kuzitumia kutokana na kutozitambua kwa ufasaha.