Uyui FM
Uyui FM
9 September 2025, 8:54 pm
Na Zabron G Balimponya
Wakili wa Kujitegemea kutoka Chama cha Mawakili Tanganyika, Akram Magoti amesema kuwa matumizi ya silaha yasiyozingatia sheria kanuni na utaratibu kutoka kwa msajili wa silaha ni kosa kisheria hali ambayo inaweza kusababisha mmiliki kufutiwa leseni.
Wakili Akram amesema hayo wakati akizungumza na UFR ambapo amesisitiza,zipo adhabu hutolewa kwa mmliki anapo kiuka maelekezo ya msajili wa silaha.

Wakili Akram Magoti akizungumza na mwandishi wa habari wa Uyui FM Radio
Baadhi ya wakazi wa Tabora wametoa maoni yao wakiwaomba wamiliki wa silaha kuzitumia vizuri bila kuhatarisha maisha ya watu wasiokuwa na hatia.
Kwa mjibu wa Wakili wa Kujitegemea kutoka Chama cha Mawakili Tanganyika, Akram Magoti kabla ya kutumia silaha kwa ajili ya kujilinda ni vyema kutumia njia ya kawaida ili kuepuka hatari ya kutumia nguvu kubwa kwa jambo linalohitaji nguvu ndogo