Uyui FM

Ukatili wa kingono unavyowaathiri watu wenye changamoto ya afya ya akili

5 August 2026, 1:51 pm

Mtangazaji wa UFR Nicolaus Mwaibale akizungumza na Bi. Asha Banka. Picha na Julius Julius

Makala hii inaelezea kuhusu ukatili wa kingono wanaofanyiwa Wasichana wenye matatizo ya afya ya akili.

Na Zaituni Juma akishirikiana na Nicolaus Mwaibale

Msichana mwenye umri wa miaka 16(mwenye tatizo la afya ya akili) mkazi wa Manispaa ya Tabora alifanyiwa ukatili wa kingono uliosababisha kupata ujauzito na kisha kujifungua mtoto kwa njia ya upasuaji.

Bibi wa Binti huyo, Asha Juma Banka amesema Mjukuu wake alizaliwa mwaka 2011 akiwa na tatizo la afya ya akili na alilazimika kumlea baada ya mama yake mzazi kumuachia jukumu la malezi akiwa bado mdogo.