Uyui FM
Uyui FM
11 November 2024, 4:38 pm

Mradi wa EPPCO utagharimu zaidi ya shilingi milioni 912 hadi kukamilika kwake
Na Zaituni Juma
Serikali ya mkoa wa Tabora imesema kuwa mradi wa EPPCO unaoratibiwa na shirika la Caritas Tabora utakwenda kuwanufaisha wananchi kwa kurahisisha upatikanaji wa huduma ya maji kwa urahisi.
Katibu tawala wa mkoa wa Tabora Daktari John Mboya amesema hayo wakati wa uzinduzi wa awamu nyingine ya mradi huku akimsisitiza mratibu wa mradi huo kukaa kwa pamoja na wakuu wa idara husika ili utekelezaji wake ulete tija kwa jamii.

Awali mratibu wa mradi wa EPPCO unaoratibiwa na shirika la Caritas Tabora Korduni Titina amesema katika utekelezaji vitachimbwa visima vitano vipya,ukarabati wa visima 15 na ujenzi wa marambo matano ya kunyweshea mifugo.

Kwa upande wao mganga mkuu wa mkoa wa Tabora Honorata Rutatinisibwa na meneja wa RUWASA mkoa wa Tabora mhandisi Hatari Kapufi wametoa ushauri wao katika utekelezaji wa mradi huo.
Nae mkuu wa makazi ya wakimbizi Ulyankulu Jumanne Singani ameeleza umuhimu wa mradi huo ambao umekuwa ukitekelezwa kwa awamu tofauti.
Mradi wa EPPCO umelenga kuimairsha amani na mshikamano kwa jamii zinazoishi katika eneo la makazi ya Ulyankulu na vijiji jirani ikiwemo vya Mgelela na Songambele mkoani Tabora.