Uyui FM

Watumishi washauriwa kujipanga kabla ya kustaafu

9 September 2025, 8:41 pm

Na Zabron G Balimponya

Imeelezwa kuwa kabla ya kufikia muda wa kustafu kazi ni vizuri kujiwekea mipango ya hakiba ya fedha pamoja na kujiandaa kisaikolojia ikiwa ni pamoja na kujiepusha na ulevi ili kujiweka vyema katika maisha ya uzeeni

Hayo yameelezwa na Afisa kazi mfawidhi mkoa wa Tabora Robert NkungweNkungwe wakati akizungumza na UFR ambapo amebainisha kuwa baadhi ya wastafu husubilia fedha ya mafao ya uzeeni ili kutengeneza maisha jambo ambalo sio sahihi

Afisa kazi mfawidhi mkoa wa Tabora Robert NkungweNkungwe akizungumza na mwandishi wa habari wa Uyui FM Radio

Sauti ya Afisa kazi mfawidhi mkoa wa Tabora Robert Nkungwe

Baadhi ya wazee Tabora wametoa maoni yao wakieleza sababu zinazo fanya wastafu kupitia wakati mgumu katika uzee wao huku wakisisitiza kuwa fedha ya mafao haitakiwi kutumika katika miradi bali ni fedha ya kutumia taratibu.

Sauti za wazee wa Tabora

Kwa mjibu wa Afisa kazi mfawidhi mkoa wa Tabora Robert Nkungweumri wa kustafu kazi huanzia miaka 60 hadi 65.