Uyui FM

INEC yaweka mazingira rafiki kwa wenye mahitaji maalum uchaguzi mkuu

9 September 2025, 9:51 pm

Na Zabron G Balimponya

Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Tabora Mjini, Paschal Richard Matagi amewatoa hofu Watu Wenye Ulemavu mkoani Tabora kwa kuwa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi imejiandaa kuhakikisha watu wote wenye mahitaji maalum wanapata huduma stahiki kulingana na hali zao.

Katika mahojiano maalum na UFR, Matagi amesema kuwa tayari wamepokea vifaa wezeshi kwa wenye ulemavu na watahakikisha wanatoa mafunzo kwa makarani wa Uchaguzi Mkuu ili kuhakikisha hakuna changamoto yoyote katika mchakato wote wa uchaguzi.

Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Tabora Mjini Paschal Richard Matagi akifanya mahojiano na UFR

Sauti ya Paschal Richard Matagi

Kwa upande wao baadhi ya Watu Wenye Ulemavu mkoani Tabora Pili Kassimu na Frank Kishimba wameiomba Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi kuhakikisha uwepo wa vifaa wezeshi na mazingira rafiki yatakayofanikisha kushiriki kikamilifu katika mchakato wa uchaguzi.

Sauti ya Pili Kasimu na Frank Kishimba

Uchaguzi mkuu wa Rais Ubunge na Diwani unatarajia kufanyika ifikapo October 29, 2025 huku vyama mbalimbali vya siasa vikiwania nafasi hizo