Uyui FM

Polisi waitaka jamii kushiriki mapambano dhidi ya ukatili

25 November 2026, 9:34 pm

Mkuu wa Polisi Jamii Mkoa wa Tabora, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Mahemba Kavalambi. Picha na Julius Julius

Jamii ya Tabora kutoa taarifa na kushiriki kikamilifu katika kupambana na ukatili wa kijinsia.

Na Julius Julius

Mkuu wa Polisi Jamii Mkoa wa Tabora, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Mahemba Kavalambi, ameitaka jamii kushiriki kikamilifu katika mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia kwa kutoa taarifa za vitendo hivyo.

ACP Kavalambi ametoa wito huo leo Novemba 25, 2026, wakati akimwakilisha Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, ACP Twaha Lulengelule, katika ufunguzi wa maadhimisho ya Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia.

Amesema mapambano dhidi ya ukatili yanahitaji ushirikiano wa jamii nzima, akisisitiza umuhimu wa kutoa elimu katika maeneo yote ili kuongeza uelewa kuhusu madhara ya ukatili katika jamii.

Sauti ya ACP Mahemba Kavalambi
Mwenyekiti wa Mtandao wa Polisi Mkoa wa Tabora, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) Edith Makweli. Picha na Julius Julius

Mwenyekiti wa Mtandao wa Polisi Mkoa wa Tabora, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) Edith Makweli, amesema katika kipindi cha siku 16 za kupinga ukatili, mtandao huo umejipanga kutekeleza shughuli mbalimbali, ikiwemo kutoa misaada kwa kaya tano zenye uhitaji katika Wilaya ya Uyui.

Aidha, amesema mtandao huo utaendelea kuwa jukwaa la kupaza sauti kwa waathirika wa ukatili na kuhamasisha wadau mbalimbali kutekeleza wajibu wao katika mapambano dhidi ya vitendo hivyo.

Sauti ya SSP Edith Makweli