Uyui FM

Wananchi Tabora watakiwa kusafisha mitaro kuzuia mafuriko

21 November 2026, 1:50 pm

Picha ni moja ya mtaro uliojaa uchafu manispaa ya Tabora. Picha na Julius Julius

Maandalizi ya kukabiliana na athari za mvua kubwa yaimarishwa Tabora

Na Elison Sabuni

Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Tabora limejiandaa kukabiliana na athari zinazoweza kusababishwa na mvua kubwa zinazotarajiwa kunyesha, kwa kuimarisha kikosi cha uokoaji majini, kufanya mazoezi ya mara kwa mara na kushirikiana na Taasisi nyingine.

Afisa Operesheni wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Tabora, Mrakibu Msaidizi Abdallah Ulutu. Picha na Elison Sabuni

Afisa Operesheni wa Jeshi hilo mkoani Tabora, Mrakibu Msaidizi Abdallah Ulutu, amesema jeshi hilo pia linaendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu namna ya kujikinga na maafa.

Sauti ya Mrakibu Msaidizi Abdallah Ulutu

Kwa upande wao, baadhi ya wananchi wa Tabora wametoa wito kwa jamii kuimarisha usafi wa mazingira kwa kuondoa taka kwenye mitaro pamoja kufukia mashimo yaliyo wazi.

Sauti za Wananchi

Hata hivyo wameiomba Serikali kuboresha miundombinu ya barabara ili kurahisisha maji kupita kwa urahisi kwenye mitaro.