Uyui FM

Mashindano ya kula kunywa kupita kiasi yatajwa kuhatarisha maisha

23 October 2026, 2:23 pm

Afisa Lishe kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tabora Kitete, Johana Ernesti. Picha na Mohamed Habibu

Kula chakula na kunywa vinywaji kwa kasi kunaweza kuhatarisha afya ya binadamu, ikiwemo kuongeza hatari ya kukabwa na chakula

Na Mohamed Habibu

Afisa Lishe kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tabora Kitete, Johana Ernesti, amebainisha madhara yanayoweza kujitokeza kwenye mashindano ya kula chakula na kunywa vinywaji kwa kasi, akisema yanaweza kusababisha madhara makubwa kiafya na hata kifo.

Ernesti amesema kula na kunywa kwa haraka kunaweza kusababisha chakula au kinywaji kuingia kwenye njia ya hewa badala ya njia ya chakula na kusababisha madhara, hivyo amewataka wananchi kuepuka mashindano hayo.

Sauti ya Afisa Lishe, Johana Ernesti
Afisa Maendeleo ya Michezo wa Manispaa ya Tabora, Arnold Jeremia. Picha na Mohamed Habibu

Afisa Maendeleo ya Michezo wa Manispaa ya Tabora, Arnold Jeremia, amesema manispaa hiyo haijapokea maombi ya vibali wala kushuhudia mashindano hayo yakifanyika, huku akisisitiza umuhimu wa kuzingatia sheria, taratibu na kanuni katika kuandaa mashindano.

Sauti ya Afisa Maendeleo ya Michezo Arnold Jeremia
Mwenyekiti wa Mtaa wa Mrimani, Kata ya Ng’ambo, Elizabeth Andrea. Picha na Mohamed Habibu

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Mtaa wa Kizigo, Grayson Samweli, na Mwenyekiti wa Mtaa wa Mrimani, Kata ya Ng’ambo, Elizabeth Andrea, wamewaasa wananchi kuepuka mashindano ya kula na kunywa kwa kasi pamoja na vitendo vingine hatarishi, ikiwemo kufanya mashindano ya kuendesha pikipiki kwa namna inayoweza kuhatarisha maisha.

Sauti ya Wenyekiti wa Mtaa wa Grayson Samweli na Elizabeth Andrea
Mwananchi Nicolaus Pascal. Picha na Mohamed Habibu
Sauti za Wananchi