Uyui FM

NSSF yakabidhi vifaa saidizi vya milioni 1.2 Hospitali ya Kitete

7 October 2026, 5:09 pm

Mwakilishi kutoka NSSF- Tabora akikabidhi vifaa Saidizi. Picha na Julius Julius.

Utoaji wa vifaa saidizi kwa watoto wenye changamoto ya utindio wa ubongo ni matokeo ya wazo lililotolewa na Uongozi wa Hospital ya Kitete ili kuwasaidia watoto hao kupata tiba ya viungo na mazoezi kwa urahisi.

Na Zaituni Juma

Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii -NSSF mkoa wa Tabora umekabidhi vifaa saidizi vyenye thamani ya Shilingi milioni 1 na laki 2 Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Tabora Kitete, kwa lengo la kusaidia watoto wenye changamoto ya utindio wa ubongo.

Akizungumza wakati wa makabidhiano, Afisa Utawala wa NSSF mkoa wa Tabora, Sosten Mtena, aliyemwakilisha Meneja wa NSSF mkoa, amesema vifaa hivyo vitasaidia kuboresha huduma za tiba na mazoezi kwa watoto wenye mahitaji maalum.

Sauti ya Sosten Mtena

Kaimu Mganga Mfawidhi Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Tabora Kitete, Swaumu Kimaro, ameishukuru NSSF kwa msaada huo uliowezesha kupatikana kwa viti 20 vitakavyotumika katika tiba ya mazoezi inayotolewa kwa watoto hao.

Daktari Swaumu Kimaro akizungumza na UFR. Picha na Julius Julius
Sauti ya Daktari Kimaro

Baadhi ya wazazi wa watoto wenye changamoto ya utindio wa ubongo wameipongeza NSSF kwa ushirikiano wake na Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Tabora – Kitete.

Mzazi wa mtoto mwenye utindio wa ubongo akitoa shukurani kwa NSSF. Picha na Julius Julius