Uyui FM

Jamii yahimizwa kulinda haki za mtoto wa kike

16 October 2026, 7:10 pm

Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Tabora, Neema Kapesa. Picha na Julius Julius

Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kike yanayoadhimishwa Oktoba 11 ya kila mwaka yatumike kwa jamii kulinda haki za mtoto wa kike na kumkinga dhidi ya vitendo vya ukatili.

Na Julius Julius

Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Tabora, Neema Kapesa ameitaka jamii kuzingatia haki za msingi za mtoto wa kike, kutambua changamoto zinazomkabili na kuweka mikakati madhubuti ya kumlinda dhidi ya vitendo vya ukatili.

Kapesa ametoa wito huo Oktoba 15, 2026, wakati akimwakilisha Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Tabora, Dkt. John Pima, kwenye kilele cha maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kike yaliyofanyika viwanja vya Nanenane, Manispaa ya Tabora.

Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Tabora, Neema Kapesa. Picha na Elson Sabuni
Sauti ya Neema Kapesa

Mkuu wa Kitengo cha Dawati la Jinsia na Watoto wilayani Tabora, Mkaguzi wa Polisi Meshack Sanga, ametoa wito kwa watoto kuripoti mara moja kwenye mamlaka husika wanapofanyiwa vitendo vya ukatili.

Mkaguzi wa Polisi, Meshack Sanga. Picha na Julius Julius
Sauti ya Mkaguzi wa Polisi, Meshack Sanga

kwa niaba ya watoto waliohudhuria maadhimisho hayo Joyce Said mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Ipuli, amesema watoto wako tayari kuchukua hatua za kujilinda dhidi ya vitendo vya ukatili, licha ya kukabiliwa na changamoto mbalimbali zinazoanzia katika ngazi ya familia.

Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Ipuli, Joyce Said. Picha na Julius Julius
Sauti ya Mwanafunzi

Naye Diwani wa Kata ya Ipuli, Juma Mollo, amesisitiza kuwa jukumu la kuwalinda watoto si la walimu pekee, bali ni wajibu wa kila mmoja.

Diwani wa Kata ya Ipuli, Juma Mollo. Picha na Julius Julius
Sauti ya Diwani Juma Mollo