Uyui FM

Polisi yawataka Abiria kuripoti Madereva wanaohatarisha usalama wao

19 October 2026, 8:16 pm

Afisa Mnadhimu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Makao Makuu, ACP Desdery Rugimbana. Picha na Julius Julius

Zoezi la ukaguzi wa ghalfa na utoaji wa elimu ni juhudi za kuhakimisha abiria wanatambua wajibu wao wa kuchukua hatua wanapobaini ukiukwaji wa sheria za usalama barabarani badala ya kusubiri madhara yatokee.

Na Julius Julius

Jeshi la Polisi limewataka abiria na wasafiri kutokaa kimya wanapobaini madereva wanaendesha magari kwa mwendo kasi au kwa uzembe, badala yake watoe taarifa ili kusaidia kuzuia ajali za barabarani.

Wito huo umetolewa leo Oktoba 19, 2026 na Afisa Mnadhimu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Makao Makuu, ACP Desdery Rugimbana wakati wa zoezi la ukaguzi wa ghafla na utoaji wa elimu kituo cha mabasi Tabora.

ACP Desdery Rugimbana akizungumza na abiria ndani ya stendi ya basi Tabora . Picha na Julius Julius

ACP Rugimbana, amesisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya abiria, madereva, kampuni za usafirishaji na Jeshi la Polisi katika kuhakikisha safari zinafanyika kwa kuzingatia usalama wa watumiani wa barabara.

Sauti ya ACP Desdery Rugimbana

Kwa niaba ya Madereva wa mabasi yaendayo mikoani Simon Christopher amesema wataendelea kufuata sheria za usalama barabarani huku akisema hatua kali zichukuliwe kwa madereva wanaovunja sheria hizo.

Dereva wa basi Simon Christopher. Picha na Michael Samwel
Sauti ya Simon Christopher

Kwa upande wa abiria Felista Ngasa amesema wataendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa pindi madereva watakapo kiuka sheria za barabarani.

Abiria Felista Ngasa. Picha na Michael Samwel
Sauti ya Felista Ngasa