Uyui FM
Uyui FM
28 October 2026, 7:49 pm

Wapangaji na wapangishaji wametakiwa kuingia mikataba ya maandishi inayobainisha kiasi cha kodi, muda na utaratibu wa malipo ili kulinda haki zao na kuepusha migogoro.
Na Mohamed Habibu
Wakili wa kujitegemea mkoani Tabora Kanani Chombala, amewataka wapangaji na wapangishaji wa nyumba kuhakikisha wanaingia mikataba ya maandishi ili kulinda haki zao na kuepusha migogoro inayoweza kujitokeza.
Chombala amesema mkataba wa kupangisha unapaswa kueleza kwa uwazi kiasi cha kodi, muda na utaratibu wa malipo.
Kwa upande wao, baadhi ya wamiliki wa nyumba mkoani Tabora wamesema mikataba ya upangaji ina umuhimu mkubwa katika kulinda maslahi yao, wakieleza kuwa baadhi ya wapangaji wamekuwa wakikiuka makubaliano.
Nao baadhi ya wananchi wanaoishi katika nyumba za kupanga wameeleza kuwa hawana utaratibu wa kutumia mikataba ya maandishi, kwa sababu hawajawahi kukumbana na changamoto katika maeneo wanayoishi.