Uyui FM

Askari 15 wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wapandishwa vyeo Tabora

28 October 2026, 5:28 pm

Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Tabora, Kamishna Msaidizi Mwandamizi (SACF) Loshipay Laizer. Picha na Julius Julius

Askari 15 waliopandishwa vyeo wasisitizwa kuwa viongozi wa mfano kwa kuzingatia nidhamu, bidii na uwajibikaji, kupandishwa cheo kunaongeza majukumu na kunahitaji maboresho katika utendaji wa kazi.

Na Julius Julius

Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Tabora, Kamishna Msaidizi Mwandamizi (SACF) Loshipay Laizer, amewataka askari wa Jeshi hilo waliopandishwa vyeo kuwa viongozi wa mfano kwa wenzao kwa kuzingatia nidhamu na bidii ya kazi.

Laizer amesema hayo leo Oktoba 28, 2026 wakati akimwakilisha Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini (CGF) John Masunga, kwenye hafla ya upandishwaji vyeo iliyofanyika ofisi za Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoa wa Tabora

Amesema askari hao 15 walioapishwa wanapaswa kutambua kuwa kupandishwa cheo ni hatua ya kuongezeka kwa majukumu, hivyo wanatakiwa kubadilika katika utendaji wa kazi.

Sauti ya Loshipay Laizer

Aidha, amewataka askari hao kuendelea kutunza afya zao ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.

Askari wa jeshi la zimamoto na uokoaji waliongezewa vyeo na baadhi ya viongozi wa jeshi hilo. Picha na Julius Julius

Laizer pia ametoa wito kwa askari ambao bado hawajapandishwa vyeo kuendelea kufanya kazi kwa bidii na nidhamu ya hali ya juu.

Sajenti Stephano Kombo. Picha na Julius Julius

Akizungumza kwa niaba ya askari walipandishwa vyeo, Sajenti Stephano Kombo,ameishukuru Serikali na uongozi wa Jeshi hilo, huku akiahidi kuendelea kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu.

Sauti ya Sajenti Stephano Kombo.