Uyui FM

Kanda ya Magharibi watakiwa kufuatilia taarifa za El Niño

12 October 2026, 12:37 pm

Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wakifanya zoezi la uokoaji bwawa la Igombe.Picha na Elson Sabuni

“Bado mikoa ya Kanda ya Magharibi haujatoka utabiri ila lazima tujiandae”

Na Elson Sabuni

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania – TMA Kanda ya Magharibi imewataka wananchi kutopuuza uwezekano wa mabadiliko ya mwenendo wa mvua yanayoweza kuchangiwa na El nino.

Mtaalamu wa Hali ya Hewa kutoka (TMA) Kanda ya Magharibi, Sudi Kisama amesema El Niño inaweza kuchangia mvua kuanza mapema katika mikoa ya Kanda ya Magharibi, ambayo kwa kawaida huanza mwezi Novemba.

Mtaalamu wa TMA Kanda ya Magharibi, Sudi Kisama akizungumza na UFR. Picha na Elson Sabuni
Sauti ya Sudi Kisama

Kisama ametoa wito kwa wakulima na wananchi kujiandaa kulingana na mwenendo wa hali ya hewa.

Sauti ya Kisama

Kwa upande wao, wananchi Manispaa ya Tabora wameeleza namna walivyojiandaa kuelekea msimu wa mvua za masika.

Baadhi ya Wananchi wa Igombe. Picha na Elson Sabuni
Sauti za Wananchi

Hayo yanajiri baada ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) kutoa tahadhari kuhusu uwezekano wa kuwepo kwa mvua za El Niño.