Uyui FM
Uyui FM
3 November 2026, 3:03 pm

Hairuhusiwi kuuza mali iliyopatikana ndani ya ndoa bila ridhaa na ushirikishwaji wa mwenza.
Na Mohamed Habibu
Wakili wa kujitegemea mkoani Tabora, Kilingo Hassani, amesema mwenza haruhusiwi kuuza mali iliyopatikana ndani ya ndoa bila kumshirikisha mwenzake.
Akizungumza na UFR, Wakili Kilingo amesema mwenza aliyeathirika anaweza kuwasilisha malalamiko katika mamlaka husika kulingana na aina ya mali iliyouzwa.

Wakizungumzia suala hilo, baadhi wananchi wamesema kuwa wanandoa wanapaswa kuepuka migogoro inayotokana na umiliki na usimamizi wa mali za familia.
Wakili wa kujitegemea Mkoani Tabora, Kilingo Hassani amewashauri wanandoa kushirikishana katika maamuzi kuhusu mali walizopata ndani ya ndoa ili kuepuka migogoro isiyo ya lazima.