Uyui FM
Uyui FM
27 October 2026, 7:47 pm

Serikali imeelekeza kuondolewa kwa wavamizi wa hifadhi za barabara kulinda miundombinu hiyo
Na Julius Julius
Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) mkoa wa Tabora, Eng. Rafael Mlimaji, amesema maelekezo ya Serikali nikuwaondoa wavamizi wa hifadhi za barabara, akieleza kuwa nyumba na mabanda 602 tayari yamebainishwa kuwa ndani ya maeneo hayo.
Mlimaji amesema hayo leo Oktoba 27, 2026 wakati akizungumza na UFR huku akiwataka wananchi walio katika maeneo ya hifadhi ya barabara kuondoa shughuli zao kabla ya kuchukuliwa hatua za kisheria.
Amesema kwa mujibu wa sheria, hifadhi ya barabara ni mita 22.5 kutoka katikati ya barabara kwenda kila upande.
Aidha, amesema suala la fidia litazingatia mipaka ya hifadhi za barabara na mipango miji iliyopo, akieleza kuwa wananchi waliovamia maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya hifadhi ya barabara hawatastahili kupewa fidia.
Baadhi ya wafanyabiashara Manispaa ya Tabora wametoa maoni tofauti kuhusu agizo la Serikali la kuondoa mabanda yaliyopo kwenye hifadhi za barabara.