Uyui FM
Uyui FM
12 October 2026, 3:26 pm

Siku ya Wazee Duniani inayoadhimishwa Oktoba 01 ya kila mwaka ni fursa ya kuthamini mchango wa wazee na kuhakikisha wanapata huduma na heshima wanayowastahili.
Na Mwanne Jumaa na Samir Salum
Jamii imetakiwa kutowatelekeza wazee na badala yake kuhakikisha wanapata mahitaji muhimu ikiwemo, huduma za afya na ulinzi dhidi ya unyanyasaji.
Akizungumza na UFR kwenye kipindi cha Kifungua Kinywa, Afisa Ustawi wa Jamii wa Manispaa ya Tabora, Nehemia Steven, amesema jukumu la kuwahudumia wazee linapaswa kuanzia katika ngazi ya familia kwa kuwapatia chakula, malazi na huduma nyingine muhimu.