Uyui FM
Uyui FM
20 October 2026, 5:44 pm

“Mafanikio hayo ni sehemu ya matokeo ya moja kwa moja ya kampeni ya “Ongea na Kamanda”.
Na Julius Julius
Jeshi la Polisi Mkoa wa Tabora linawashikilia watu watatu kwa tuhuma za kuwa sehemu ya mtandao wa kuuza na kusambaza dawa za kulevya ikiwa ni sehemu ya matunda ya Kampeni ya “Ongea na Kamanda”.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Oktoba 20,2026 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Twaha Lulengelule amesema kati ya watuhumiwa hao watatu waliokamatwa, Mmoja amekutwa akiwa na kete 26 zinazodhaniwa kuwa ni Heroin pamoja na vifaa vya kufungashia.

Aidha, mtuhumiwa huyo amekutwa akiwa na dawa aina ya Apcalis ambayo inadaiwa kutibu tatizo la nguvu za kiume.
Jeshi la Polisi limewataka wananchi kutumia fursa ya Kampeni ya “Ongea na Kamanda” na Kampeni nyingine zinazoendelea kupitia Falsafa ya Polisi Jamii kutoa taarifa dhidi ya uhalifu na wahalifu ikiwemo mtandao wa dawa za kulevya.