Uyui FM
Uyui FM
19 October 2026, 7:18 pm

Abiria kushiriki kudhibiti ajali za pikipiki kwa kuepuka kupanda pikipiki zisizozingatia sheria za usalama barabarani
Na Mohamed Habibu
Mwenyekiti wa Umoja wa Maafisa Usafirishaji mkoa wa Tabora, Mrisho Shime, amesema abiria wana nafasi kubwa katika kudhibiti ajali za pikipiki kwa kukataa kupanda vyombo vinavyoendeshwa kinyume cha sheria za usalama barabarani.
Akizungumza katika kipindi cha Kifungua Kinywa, Shime amesema baadhi ya abiria huchangia ajali kwa kuwashinikiza madereva kuendesha kwa mwendo kasi, huku wengine wakikubali kupanda pikipiki zinazoendeshwa na madereva wasiovaa kofia ngumu.
Amesisitiza kuwa abiria wanapaswa kudai usalama wao kwa kuhakikisha dereva anazingatia mwendo unaotakiwa barabarani, akieleza kuwa hatua hiyo inaweza kusaidia kupunguza ajali, vifo na ulemavu wa kudumu.