Uyui FM
Uyui FM
11 November 2026, 9:28 am

TRA Mkoa wa Tabora yavuka lengo la ukusanyaji wa mapato kwa asilimia 118.94 katika kipindi cha Julai hadi Oktoba mwaka 2026.
Na Julius Julius
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Tabora imevuka lengo la ukusanyaji wa mapato kwa asilimia 118.94 katika kipindi cha Julai hadi Oktoba mwaka 2026.
Akizungumza Novemba 10, 2026, katika kikao cha Jukwaa la Wadau wa Kodi kilichofanyika Hoteli ya JM Manispaa ya Tabora, Meneja wa TRA Mkoa wa Tabora, Alex Katundu, amesema mafanikio hayo yametokana na ushirikiano wa wadau mbalimbali.

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Mohamed Nassoro Hamdan, ameitaka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuongeza nguvu katika utoaji wa elimu ya kodi kwa makundi yote ya walipakodi ili kupunguza malalamiko.

Aidha Meneja wa Mlipa Kodi Makao Makuu ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Herieth Mteki amesema mabadiliko ya sheria za kodi kwa mwaka wa fedha 2026/2027 yanatoa fursa kwa wafanyabiashara kusajiliwa na kupata namba ya utambulisho wa mlipakodi (TIN) bila malipo.
Amesisitiza kuwa hatua hiyo inalenga kuwasaidia wafanyabiashara kuanzisha na kukuza biashara zao hatua kwa hatua, huku TRA ikiendelea kuwafikia na kutoa huduma pamoja na elimu ya kodi.