Radio Jamii Kilosa

Wananchi watakiwa kuongeza unywaji wa maziwa kwa afya bora

3 June 2025, 6:58 pm

Afisa Ushirika Kilosa Ndg Robert Lucian akizungumzia suala la unywaji maziwa katika studio za Redio Jamii Kilosa. Picha na Asha Madohola

Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), mtu mzima anapaswa kunywa angalau lita 200 za maziwa kwa mwaka. Hata hivyo, takwimu za hivi karibuni zinaonyesha kuwa wastani wa unywaji wa maziwa kwa Mtanzania ni lita 67.2 kwa mwaka, kiwango ambacho ni chini ya mapendekezo ya WHO.

Na Beatrice Majaliwa

Wananchi na wadau mbalimbali wilayani Kilosa wameeleza wasiwasi wao kuhusu mwamko mdogo wa unywaji wa maziwa, wakisisitiza umuhimu wa elimu kwa jamii kuhusu faida za lishe hiyo muhimu.

Mkazi wa Kilosa Bi Shanila Matingisa

Wakizungumza na Redio Jamii Kilosa, baadhi ya wananchi wamesema kuwa sababu kuu ya unywaji mdogo wa maziwa ni ukosefu wa elimu na kipato duni miongoni mwa wananchi.Bi Shanila Matingisa.

Sauti ya Bi Shanila Matingisa akizungumza

Naye Bi Neema Jofrey amesema kuwa mazoea ya kutokunywa maziwa tangu utotoni yamechangia watu wengi kutokuona umuhimu wake hata wakiwa watu wazima.

Sauti ya Mkazi wa Kilosa Bi Neema Jofrey

Ameongeza kuwa elimu zaidi inahitajika ili kuongeza mwitikio wa unywaji wa maziwa.

Sauti ya Mkazi Bi Neema Jofrey

Kwa upande wake, Afisa Ushirika wa Wilaya ya Kilosa, Bw. Robert Lucian, amesema kuwa idara ya Mifugo imejipanga kutoa elimu kwa wananchi kuhusu faida za unywaji wa maziwa, kuzungumza na wafugaji ili kupata takwimu sahihi za uzalishaji wa maziwa, na kuwashauri wafugaji kujiunga na vyama vya ushirika wa wauza maziwa.