Pambazuko FM Radio

Wakulima wapatiwa mafunzo ya kilimo bora kwa mazao ya Miwa na Mpunga – Ifakara

15 April 2023, 10:00 pm

Wakulima wakifuatilia maelekezo juu ya kilimo bora ( Picha na Isidory Mtunda)

Wakulima wa halmashauri ya mji wa Ifakara wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro, Aprili 14, 2023 wamepatiwa mafunzo juu ya Ulimaji bora wa Miwa, Mpunga na matumizi bora ya zana za kilimo kutoka Kampuni ya EFTA Tanzania Ltd.

Na; Isidory Mtunda

Akizungunza na Pambazuko fm mkurugenzi wa operesheni kutoka EFTA, bwana Leonsi Malamsha amesema mada zingine zilizofundishwa ni pamoja na; Kilimo bora cha kisasa na mabadiliko ya tabia nchi.

Sauti ya Leonsi Malamsha

Wakulima Skola Shushu, Said Kimeta na Mary Mwandu wamefurahishwa na maonesho ya zana za akilimo ambapo wamevutiwa zaidi na jembe la Mod Bolt Plough, ambalo linafanana na Jembe la Ng’ombe.

Jembe aina ya Mod Bolt Plough – ( Picha na; Isidory Mtunda)

Sauti za wakulima

Afisa mauzo kutoka EFTA bwana Boniface Elias Mollel amesema jembe aina ya Mold Bolt Plau linachimba vizuri na kuruhusu maji kupenya chini ya ardhi na pia halina spea nyingi ukilinganisha na jembe la aina ya Diski Plau ambalo wakulima wengi hutumia.

Sauti ya bwana Mollel

Trekta likiwa katika majaribio ya kulima kwa kutumia Mold Bolt Plough katika shamba darasa ( Picha na; Isidory Mtunda)

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Kilombero wakili Danstan Kyobya mgeni rasmi katika mafunzo hayo, amewashauri wakulima hao kutengeneza  mashine ndogo ndogo za Sido kwaajili ya kukoboa mpunga na kuweka katika madaraja ili kuongeza thamani ya mazao yao.

Sauti ya mkuu wa wilaya – D. Kyobya

Mafunzo hayo yamefanyika Ifakara mjini, katika ukumbi wa Vijana jirani na Parokia ya Ifakara, ambapo wakulima zaidi ya mia sita wamehudhuria mafunzo hayo.