Pambazuko FM Radio

Ufugaji wa Nyuki huzuia uharibifu wa rasilimali Misitu na Mazingira

8 February 2023, 2:37 pm

Na Katalina Liombechi

Ufugaji Nyuki Wilayani Kilmbero imetajwa kuwa shughuli Mojawapo rafiki kwa uhifadhi endelevu wa Rasilimali za Misitu na Mazingira kwa Ujumla.

Afisa Nyuki Halmashauri ya Mlimba Wilayani Kilombero bwana John Mlulu ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuelezea umuhimu wa uhifadhi wa rasilimali misitu na namna wanavyohamasisha ufugaji wa Nyuki na faida zake.

Hili ni moja ya eneo la ufugaji wa Nyuki katika Halmashauri ya Mlimba{Picha na Katalina Liombechi}

Amesema ufugaji wa Nyuki umesaidia kwa kiasi kikubwa kuhifadhi rasilimali misitu kwani wananchi wengi wameacha kulima kwa kuhama hama na kuhamasika kufuga Nyuki kutokana na tija wanayoipata mara baada ya kuuza Asali,  huku akitolea mfano mafanikio kwa wananchi wa Kata ya Masagati ambapo Halmashauri hiyo kwa kushirikiana na wadau mbalimbali Wamekuwa wakiwasaidia kuwatafutia masoko.

Amezitaja faida zingine kuwa Asali hutumika kama Chakula na Dawa huku akitumia fursa hiyo kutoa wito kwa jamii kufanya ufugaji wa nyuki ili kuzuia uharibifu wa rasilimali misitu unaotokana na uvamizi,kulima ndani ya maeneo hayo,kupitisha makundi ya Mifugo na kuzuia mioto ndani ya maeneo ya Misitu.

Sauti ya Afisa Nyuki Halmashauri ya Mlimba Bwana John Mlulu akielezea faida za ufugaji Nyuki

Wakizungumza baadhi ya wanakikundi cha Ufugaji Nyuki Kata ya Idete (KIWAVIKAI) wanaelezea namna ambavyo wamekuwa wakinufaika kiuchumi kupitia ufugaji huo na namna ambavyo wamekuwa wakiungwa mkono na Wadau mbalimbali wakiwemo Wakala wa huduma za Misitu(TFS).

Modestusi Mwambaluka ni mwanakikundi wa KIWAVIKAI {Picha na Katalina Liombechi}

Afisa Misitu Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba Magai Fares Chamba amesema wamekuwa wakitekeleza majukumu kadhaa kwa kushirikiana na wadau kwa kuwapatia mafunzo kamati za mazingira ili kufanya uhifadhi wa Misitu kuwa Endelevu.

Afisa Misitu Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba Magai Fares Chamba akielezea namna wanavyowapatia mafunzo kamati za mazingira