Pambazuko FM Radio

Rc Mwasa azuia utolewaji wa vibali vya uchomaji wa mkaa

31 January 2023, 12:07 pm

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Bi Fatma Mwassa.Picha na mwananchi

“Kutokana na mabadiliko ya tabianchi ambayo inaikumba nchi yetu na Dunia kwa ujamla Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Bi Fatma Mwasa amepiga marufuku uchomaji wa mkaa na kuwataka wanaofanya shughuli hizo ,watafute shughuli zingine za kufanya”

By Elias Maganga/Isdory Mtunda

Mkuu wa mkoa wa Morogoro Fatma Mwasa amezuia utolewaji wa vibali vya uchomaji wa mkaa ambavyo kwa kiasi kikubwa ndivyo vinavyosababisha uharibifu wa mazingira.

Wananchi acheni kukata miti na uchomaji wa mkaa badala yake tumieni njia mbadala hususani matumizi ya gesi 

Bi Fatma Mwasa ametoa zuio hilo alipokuwa akizungumza na wakazi wa Halmashauri ya Mji wa Ifakara Wilayani Kilombero wakati akizindua kampeni ya upandaji miti ,ikiwa ni utekelezaji wa agizo la makamu wa Raisi Dr Philip Isdory Mpango alililolitoa januari 12 wakati wa kilele cha maadhimisho ya miaka 59 ya mapinduzi tukufu ya Zanzibar.

Bi Fatma mwassa amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Kilombero kwa kushirikiana na wakala wa huduma za misitu Tanzania{TFS]kutotoa vibali hivyo kwani uharibifu wa mazingira unazidi kushika kasi kwa watu kukata miti kwa uchomaji wa mkaa’,

Kutokana na hali hiyo amesisitiza wananchi kuacha kukata miti na uchomaji wa mkaa badala yake watumie njia mbadala hususani matumizi ya gesi na kwa wale ambao shughuli zao kubwa ni uchomaji wa mkaa watafute shughuli zingine za kufanya