Ileje FM
Ileje FM
30 October 2026, 7:48 am

Kijana huyo amekamatwa zkiwa ni siku chache tangu TANESCO ianze majaribio ya kupitisha umeme kwenye mradi mkubwa wa TAZA kipande cha iganjo hadi sumbawanga.
Na Denis Sinkonde,Momba
Wananchi wa Mtaa wa Namole, Wilaya ya Momba mkoani Songwe, wamefanikiwa kumkamata Kefasi Mtega (30), mkazi wa Chapwa, anayetuhumiwa kujihusisha na wizi wa miundombinu ya umeme katika mradi wa TAZA unaotekelezwa na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).
Mtuhumiwa huyo amekamatwa nyakati za usiku, kufuatia tuhuma za kuiba miundombinu hiyo inayotumika katika utekelezaji wa mradi huo.
Akizungumza akiwa eneo la tukio alipokamatwa mtuhumiwa huyo, Mtendaji wa Eneo hilo, Adam Bukuku, amesema alipokea taarifa kutoka kwa msamaria mwema kuhusu tukio la wizi huo, hatua iliyowezesha kufuatiliwa kwa mtuhumiwa na hatimaye kukamatwa kwake.
Kwa upande wake, Afisa Usalama wa TANESCO Mkoa wa Songwe, Juma Mauba, amethibitisha kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo na kueleza hatua zinazochukuliwa na shirika hilo katika kukabiliana na vitendo vya wizi na uharibifu wa miundombinu ya umeme.
“Mtuhumiwa huyo anapaswa kuchukuliwa kuwa mtuhumiwa hadi uchunguzi na taratibu za kisheria zitakapokamilika,” amesema Mauba.
kijana huyo amekuwa wa pili kukamatwa baada ya mwezi mmoja kupita kijana mwingine kukamatwa akiunganisha umeme kwenye nyumba za watu bila kuwa na kibali kutoka Shirika la Umeme Tanzania(TANESCO) Mkoa wa Songwe kitendo ambacho jamii inapaswa kushirikiana na shirika hilo ili watakaobainika waweze kufikishwa kwenye vyombo vya sheria